Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Simba SC itacheza hatua ya kwanza ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Ahly Tripol ya nchini Libya.
Al Ahly Tripol imewaondoa Uhamiaji FC ya Visiwani Zanzibar kwa jumla ya magoli 5-1, na kufuzu hatua ya kwanza ambapo watacheza dhidi ya Simba SC.
Mchezo wa kwanza Simba SC atakipiga ugenini Septemba 13 na mchezo wa marudiano utapigwa Dar es salaam Septemba 20, ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi.
#NTTupdates