×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SIMBA SC KULIPA GHARAMA ZA UHARIBIFU BENJAMIN MKAPA

Na Mwandishi wetu.

Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na michezo kupitia kwa Waziri wake Prof. Kabudi ameitaka klabu ya Simba SC kulipa gharama zote za uharibifu wa miundombinu ya uwanja huo uliojitokeza hapo jana kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya wenyeji Simba SC dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia ambapo Simba SC ilishinda kwa magoli 2-1.

Pia Waziri Kabudi amelitaka jeshi la polisi kuwakamata wale wote waliohusika na uharibifu huo na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.

Taarifa ya jeshi la polisi hapo jana kupitia kwa mkuu wa Jeshi wa jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne alisema kuwa viti zaidi ya 256 viling’olewa hapo jana ambapo 100 vya rangi ya machungwa na 156 vya rangi ya Bluu.

Hii ni mara ya pili kwa mashabiki wa klabu ya Simba SC kung’oa viti kwenye dimba la Benjamin Mkapa ambapo waliwahi kufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Refa.

#NTTupdates