Na Mwandishi wetu .
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza mchezo wake wa nyumbani wa hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia (FIFA) dhidi ya Niger kwa kichapo cha goli 1-0 katika dimba la New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.
Stars imesalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi E wakiwa na alama 10 huku Niger ikiwa nafasi ya 3 baada ya kufikisha alama 9.
#Tanfootball
#NTTupdates