×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TANZANIA YAPANGWA KUNDI A BAFCON 2024

Na Mwandishi wetu.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach soccer) imepangwa Kundi A kwenye fainali za Afrika za soka la ufukweni (BAFCON 2024) zitakazofayika nchini Misri kuanzia Oktoba 19 mpaka 26, 2024 kwenye fukwe za Hughada nchini humo.

Tanzania imepangwa na mataifa ya Morocco, mwenyeji Misri na Ghana kusaka bingwa wa michuano hiyo 2024, ambapo itatupa karata yake ya kwanza siku ya jumamosi Oktoba 19, 2024 dhidi ya Morocco.

Kikosi cha Tanzania kimeshawasili Misri kujiandaa na michuano hiyo huku kikiratajiwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

#NTTupdates