×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TARURA HAIHUSIKI NA BOMOABOMOA YA KUTA ZA NYUMBA ZA WAKAZI WA OLOSIVA

Na Mwandishi wetu.

Mnamo Aprili 12, 2025 zaidi ya wananchi 200 wa kata ya Olisiva mkoani Arusha waliendesha bomoabomoa ya kuta za nyumba kwa madai ya kupanua barabara na kufanya uharibifu wa mali za watu ambao walidai kutokushirikishwa juu ya uwepo wa mpango huo wa upanuzi wa barabara hiyo.

Wakazi wa eneo hilo walimtuhumu mwenyekiti wa kitongoji cha Olisiva, Loshie Jonasi, Diwani wa Kata hiyo Erick Samboja pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Charles Sikoy kwa kuongoza bomoabomoa hiyo iliyoleta sintofahamu kwa baadhi ya wananchi wa eneo hilo.

Akiongea na vyombo vya habari leo Aprili 15, 2025 Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) mkoa wa Arusha, Mhandisi Nicolous Francis amesema kuwa Tarura haihusiki na mpango huo wala haikutuma watu hao kufanya kitendo hicho cha kubomoa kuta za nyumba za watu hivyo wale wote waliohusika na kitendo hicho wanahesabika kama wahalifu wengine na hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi yao.

Amesisitiza kuwa wananchi hao wako kinyume na sheria na kusema kuwa endepo wangetaka kuongeza upana wa barabara hiyo wangelete maombi Ofisini ili Tarura waiweke barabara hiyo kwenye mpango wa mwaka wa fedha 2025/2026 .

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kitongoji cha Olisiva Loshie Jonasi amesema kuwa waliohusika na bomoabomoa hiyo ni wananchi na sio viongozi kama inavyodaiwa na wananchi hao.

#NTTupdates.