×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

THRDC KUJA NA TAMKO LA TISHIO UTEKAJI WA WATOTO NCHINI

Na Mwandishi wetu.

MTANDAO wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), wameanza Mkutano Mkuu wa Wawakilishi wa Kanda ya Ziwa Magharibi na Mashariki lengo likiwa ni kujadili na kubaini hali ya utekelezaji wa shughuli za utetezi wa haki za binadamu, sambamba na changamoto wanazokumbana nazo.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo mapema leo, Mratibu wa Mtandao huo Taifa, Onesmo Ole Ngurumwa amesema wanatarajia kubaini na kufikia muafaka juu ya namna sahihi ya kushughulikia matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini ambayo yanatokea.

Amesema pamoja na mambo mengine Waratibu pamoja na Wajumbe wa Kanda hizo wanatarajia kujadili na kuja na tamko la pamoja kuhusu hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na tishio la kutekwa kwa watoto linaloendelea hapa nchini.

“Tutajua yale wanayopitia katika utekelezaji wa kazi zao sambamba na wao kama watetezi wa haki za binadamu wataeleza juu ya tatizo la utekaji wa watoto na wajibu wa jamii pamoja na vyombo vya usalama katika kukabiliana na tatizo hili,”amesema Ngurumwa.

#NTTUpdates