
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ili kutoa fursa kwa wananchi na waumini wa dini ya Kiislam kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr.
Miongoni mwa maeneo ambayo ulinzi umeimarishwa ni Uwanja wa mpira wa miguu Nyamagana ambako ibada inaswaliwa kimkoa, maeneo yote ya misikiti, maeneo ya kumbi za starehe na burudani, mitaa mbalimbali, na barabara zote zinazoingia na kutoka jijini Mwanza.