Na Mwandishi wetu.
Hivi ndivyo Uongozi Mpya wa Chama Cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim Rungwe ulivyowasili ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, kwenye mapokezi ya Wanachama wapya zaidi ya 3,000 ambao wamejiunga na chama hicho wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ametanguliwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Salum Mwalimu na viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Naibu Katibu Mkuu Bara Benson Kigaila na Kaimu makamu mwenyekiti Devotha Minja.