×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

USAID KUFADHILI MIRADI YA MAJI MANYARA

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Mkoa wa Manyara Queen Sendinga Julai 25, 2024 amezindiua mradi wa USAID wa Rural Evidence and Learning for Water ( REAL- Water) kupitia mfuko wa udhamini wa Ubora wa maji nchini Tanzania, mpango huu unaolenga kusaidia sekta ya maji kwa kutoa huduma ya maji vijijini na kuhakikisha usalama na maji safi kwa kuboresha mbinu za kupima na kutibu maji ili yawafikie watumiaji wote yakiwa safi na salama.

Aidha RC Sendinga ameishukuru Serikali ya ya sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwavutia wafadhili pamoja na kutenga fedha kwaajili ya uboreshaji na usambazaji wa huduma za maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.

Sambamba na hilo, ameipongeza USAID kwa kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa maendeleo yanayosaidia jamii ya watanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali kwenye sekta ya Afya, Maji na Elimu.

#NTTupdates