Na Mwandishi wetu.
Bingwa wa Dunia wa uzani wa juu wa ngumi za kulipwa na asiyepigika Aleksandr Usyk (37) raia wa Ukraine amemtwanga tena bingwa wa zamani Tyson Luke Fury (36) raia wa Uingereza kwenye pambano la raundi 12 usiku wa kuamkia leo jijini Riyadh Saudi Arabia kwenye uwanja wa Kingdom Arena na kuondoka na mikanda yote ambayo ni WBO, WBC, IBO na WBA.
Pambano hilo ambalo lilikuwa la marejeano baada ya lile la Mei 18, 2024 Fury akipoteza na kutoridhishwa na matokeo hayo na kuhitaji pambano hilo lirudiwe.
Fury ambaye amepambana mapambano 37 akishinda mapambano 34, akitoka sare pambano 1 na kupoteza mapambano mawili yote dhidi ya Aleksandr Usyk hajaridhishwa na uamuzi wa majaji kumpa ushindi mpinzani wake na kudai kuwa ameibiwa.
“Nimekuwa kwenye ndondi maisha yangu yote na huwezi kubadilisha uamuzi wowote lakini siku zote nitakuwa na hisia ngumu usipopata mtoano huwezi kujihakikishia ushindi”
“Nadhani nilishinda mapambano yote mawili, hakuna shaka akilini mwangu nilishinda pambano hilo, nadhani Usyk alipata zawadi ya Christmasi lakini si kosa la Aleksandr”
Aleksandr Usyk anaingia tena kwenye rekodi ya ambapo hadi sasa amecheza mapambano 23 akishinda yote huku 14 kwenye mapambano hayo na kuwa Bingwa asiyepigika.
#NTTupdates