×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:- (i) Bw. Salim Ramadhani Msangi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Msangi alikuwa akikaimu nafasi hiyo; na (ii) Bw. Abdul Athumani Mombokaleo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombokaleo alikuwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), anachukua nafasi ya Bw. Mussa Mbura ambaye atapangiwa majukumu mengine.

#NTTupdates