×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

UVCCM WAFANYA MATEMBEZI MAALUM KUUNGA MKONO UTEUZI WA RAIS SAMIA NA MWINYI UCHAGUZI 2025

Na Mwandishi wetu.

Vijana zaidi ya 1,000 wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamefanya matembezi maalum kuunga mkono maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika Januari 18 na 19, 2025, jijini Dodoma.

Katika mkutano huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi walipitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza baada ya matembezi hayo, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida, alisema vijana wamejipanga kuhakikisha viongozi hao wanapata kura nyingi katika uchaguzi mkuu.

Amesisitiza kuwa matembezi hayo ni ishara ya msimamo wa vijana katika kuhakikisha ushindi wa CCM.

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo, aliongeza kuwa matembezi hayo ni sehemu ya ahadi ya vijana kuunga mkono maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu. Amesema vijana wako tayari kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola na kuleta ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

Vijana walioshiriki matembezi hayo walieleza kuridhishwa na uteuzi wa viongozi hao na kuwataka wanachama wa CCM kuunga mkono maamuzi hayo.

#NTTupdates