×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

UWANJA WA NDEGE MSALATO KUANZA SEPTEMBA 2024

Na Mwandishi wetu.

WAZIRI wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege Msalato, kutapunguza msongamano wa idadi ya ndege kutua katika uwanja wa Dodoma.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo Julai 25,2024 jijini Dodoma, alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo utakaogharimu zaidi ya sh. bilioni 360 na kusema kwamba matarajio yao ni mpaka kufikia mwezi Septemba au Oktoba ndege zitaanza kutua.

Amesema kiwanja hicho ni muhimu kwa ajili ya uchumi wa nchi, na maendeleo ya Dodoma kwakuwa ni makao makuu.

“Lazima tuwe na kiwanja cha ndege cha kisasa, kiwanja hiki kitakuwa na urefu wa kilomita 3.6 na upana wa sentimita 60, maana yake kwenye category ya viwanja vya ndege hii ni 4E hivyo ndege kubwa zinaweza kutua bila matatizo.

“Amefafanua kuwa kazi kwa sasa inaendelea vizuri licha ya kuwa kipindi kilichopita kulikuwa na changamoto ya mvua lakini kwa sasa wanajiribu kumsukuma mkandarasi aweze kufanya kazi kwa haraka ili ifikapo Septemba kazi za msingi ziwe zimekamilika.

“Kwa sababu mwaka ujao Januari hali ya hewa itabadilika tena, kwa vile package hii inaenda vizuri na sisi tumejipanga ikimalizika, tutaanza kuleta ndege, tutaweka mahema ya dharura kwa ajili ya ukaguzi, ili tuweze kufanya uwanja wa Dodoma mjini uweze kupumua.

“Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato Dodoma, Meneja Miradi ya Viwanja vya Ndege TANROADS, Mhandisi Neema Mwasha amesema mradi huo umefadhiliwa na serikali ya Tanzania ikishirikiana na benki ya Maendeleo ya Afrika.

Amesema Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha miundombinu na ilisainiwa septemba 2021 kwa gharama ya Sh Bilioni 165.627 ambapo muda wa mkataba ni miezi 36 pamoja ja miezi 12 ya muda wa uangalizi.

#NTTupdates