Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumuongezea mkataba mlinzi wao wa kati Virgil Van Dijk (33) raia wa Uholanzi, ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka klabuni hapo hadi 2027.
Mlinzi huyo ambaye amkataba wake ulikuwa unamalizika mwisho mwa msimu huu, huku klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia ilionyesha nia ya kumuhitaji lakini sasa nyota huyo anaungana na mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Misri Mo Salah ambaye pia amesaini mkataba wa miaka miwili na kusalia klabuni hapo.
Msimu huu hadi sasa Virgil Van Dijk, amecheza michezo 44 akifunga magoli 4 na kutoa assist 1 kwenye mashindano yote ambayo Liverpool imeshiriki hadi sasa.
#NTTupdates