×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

“VIFO VYA MAMA NA MTOTO VIMEPUNGUA NCHINI” – MKURUGENZI MSD

Na Mwandishi wetu.

Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) Mavere Tukai amesema kupungua kwa vifo vya watoto wachanga na akina mama wakati wa kujifungua kumechangiwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye Idara ya afya.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita ambapo amesema vifo vya mama wanaojifungua vimepungua Kutoka 556 mwaka 2016/2017 hadi vifo 104 mwaka 2021/2022.

“Mafanikio hayo siyo ya kawaida,fikiria unapungiza kwa zaidi ya robo kwa hiyo matokeo yake ni kwamba kama walikuwa wanakufa 500 wanakufa 100 ,mafanikio haya ni kwa sababu ya miradi ambayo aliianzisha Rais Samia kuhakikisha inaokoa mama na mtoto,” amesema.

Aidha amesema kuwa MSD imeshiriki katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kupitia mradi uitwao SIMCO uliolenga kuondoa athari za uzazi anazopata mama wakati wa kujifungua.

“Kwa hiyo kupitia mradi huo, tulipeleka vifaa tiba ,mashine kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Moja,huu ni Mradi ambao ulianza tangu 2019 lakini mafanikio makubwa zaidi tumeanza kuyaona kuanzia 2921/2022 mpaka mwaka Jana,”amesema.

Akizungumza upatikanaji wa bidhaa za afya ameisema Bohari ya dawa imeendelea kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vyakutolea huduma za afya.

#NTTupdates