
Na Mwandishi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohammed Ali Kawaida amemuhakikishia Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Vijana wote nchi nzima wapo Tayari kukipigia kura kwa Chama cha Mapinduzi pamoja na kudumisha Amani, Umoja na mshikamano kipindi chote cha zoezi hilo.
Mwenyekiti ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika viwanja vya CCM Kirumba uliopo Mkoani Mwanza.



#NTTupdates