×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

VIJANA WATAKIWA KUTOTUMIKA VIBAYA KIPINDI CHA UCHAGUZI

Na Mwandishi wetu.

Vijana wametakiwa kutotumika na wanasiasa, wanaharakati pamoja na watia nia katika nafasi mbalimbali za uongozi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika October 29 Mwaka huu na badala yake wawe sehemu ya ulinzi wa nchi sambamba na kudumisha amani na mshikamano.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Ilemela Shekhe Mohamed Uledi wakati wa dua maalum iliyofanyika katika Kata ya Kiseke wilaya ya Ilemela jijini Mwanza iliyolenga kuliombea Taifa amani, kuwaombea Viongozi wa Serikali na viongozi wa dini ya kiislamu katika mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuhimarisha amani hapa nchini lupitia dua na sala.

Katika hatua Nyingine ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu hili kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika katika hali ya amani na utulivu.

Kwa upande wake Qadhi wa Wilaya ya Ilemela Shekhe Hassan Mchondo amesema, kuwa haki huletwa na uwepo wa amani ndani ya nchi huku akisisitiza jamii kuendelea kuhubiri amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu pamoja na kujiweka mbali na vurugu na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Pili Juma ni mmoja kati ya baadhi ya washiriki wa dua hiyo wamewaomba viongozi wa dini kufanya dua hizo kuwa endelevu kwani usaidia katika Kujenga umoja, mshikamano na kubadili mitazamo ya Vijana na badala yake kuwa chachu ya Maendeleo ya taifa.

#NTTupdates