×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WAKULIMA DODOMA WAPIGWA MSASA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA MTAMA

Na Mwandishi wetu,Dodoma.

WAKATI serikali ikiendelea kuweka mikakati mbalimbali yakuboresha sekta ya kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji wakulima wa zao la mtama wa kata ya Ikomboringa, Wilaya ya Chamwino na Iringa mvumi wameaswa kuhakikisha vikundi wanavyounda vinakua endelevu ili kunufaika na fursa zinazopatikana kama vile mikopo na uzalishaji mbegu.

Rai hiyo imetolewa na mratibu wa kilimo himilivu cha zao la mtama Actionaid Cosmas Deogratius Baoleche wakati akizungumza na wakulima hao, kwenye mafunzo yaliyoandaliwa ili kuwajengea uwezo wakulima hao pamoja na kuwaonyesha teknolojia za kilimo za kisasa, ambapo amesema uzalishaji wa mtama kwa Tanzania bado upo chini na haukidhi mahitaji ya soko, ingawa zao hilo la mtama ni fursa inayoweza kumkomboa mkulima.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima Philemon Mwaluko, lucy kwanga, richard Yoram na Monica Ndaw,i wameomba watafiti kuendelea kufanya utafiti kwa mbegu ambazo zinastahimili mabadiliko ya tabia nchi huku wakizungumza namna ambavyo mafunzo waliyoyapata kutoka Actionaid na wawezeshaji yatavyosaidia wao kuunda vikundi, na kufanya uzalishaji wenye tija kwakunufaika pamoja.

Wamesema kuwa mafunzo hayo ya kutumia teknlojia bora kama vile mbegu bora, mashine zakupura, vifaa vya kuhifadhi mazao, dawa za kudhibiti magonjwa na wadudu na teknolojia nyinginezo walizojifunza itawasaidia kupunguza upotevu wa zao la mtama kuanzia shamabani kwani Hadi kwenye kuhifadhi kwani baadhi walikua hawafamu namna teknolojia hizo zinavyoweza kurahisisha kilimo.

Naye Afisa kilimo Wilaya ya Vhamwino living kilawe, amewaasa wakulima kutumia vizuri elimu wanayopata ili kulima kwa tija, huku afisa kilimo kata ya Iringa Mvumi Deodatus Kagaluki akieleza kuwa kumekuwa na mabadiliko kwa wakulima tofauti na miaka ya nyuma na changamoto zinazojitokeza zinaendelea kufanyiwa kazi.

Naye Diwani kata ya Ikomboringa Mtemi Sefu Matonya, ametoa wito kwa Actionaid na wadau wanaofanikisha mradi huo kuhakikisha wakulima wanapata vifaa na mbegu kwa wakati.

Mradi wa kilimo himilivu cha mtama unaotekelezwa na Actionaid kwa ufadhili wa WFP moja ya malengo ya mradi huu ni kuendeleza kilimo himilivu, kinacholinda mazingira na kukuza uzalishaji kilimo kwakuzingatia kanuni za kilimo hai, ambacho kinalenga kuhakikisha mazao yanakuwa na ubora unaokubalika kwenye soko la kimataifa.

#NTTupdates