×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WALIOMWAGIA TINDIKALI MKULIMA WAHUKUMIWA JELA MAISHA

Na Mwandishi wetu.

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imewahukumu kifungo cha maisha jela watuhumiwa watano, akiwemo mwenyekiti wa kijiji na balozi, kati ya kumi waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 55 ya mwaka 2023 ya kujaribu kuua.

Watuhumiwa hao, wanadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Septemba 1, 2022, katika kijiji cha Nyamasere, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, ambapo walimvamia na kumwagia tindikali William Buyeye mkulima na mkopeshaji wa fedha katika kijiji hicho wakilenga kumuua.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Athuman Matuma amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka uliithibitishia mahakama bila shaka yoyote kuwa watuhumiwa hao watano walihusika moja kwa moja na tukio hilo la kikatili.

Aidha, amewaachia huru watuhumiwa wengine wanne baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha dhidi yao.

Kwa upande wa wakili wa Serikali, ukiongozwa na Jaynes Kiwelo, wamepongeza uamuzi wa mahakama hiyo, wakisema kuwa adhabu iliyotolewa ni ya haki na inapaswa kuwa fundisho kwa jamii.

Hata hivyo, upande wa utetezi, ukiwakilishwa na wakili Sekundi Bartholomeo, umeonyesha kutoridhishwa na uamuzi huo, ukieleza kuwa watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

#NTTUpdates