Na Mwandishi wetu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Elikana Balandya, amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu huku akisema ndio nyenzo muhimu ya kuweza kufika mbali na kutimiza ndoto walizonazo za kielimu.
Balandya ameyasema hayo, katika shule ya sekondari ya Buswelu wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilemela.
“Niwasihi kuwa na nidhamu katika masomo yenu lakini nidhamu kwa walimu na watu wote wanaowazunguka, kwani yoyote mwenye nidhamu siku zote husonga mbele” alisema Balandya.
Aidha ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa wanafunzi wa kidato cha sita waliomaliza mapema mwaka 2025 kwa ufaulu mzuri sambamba na kuwapongeza walimu kwa jitihada zao na kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu na huku akiwahimiza wanafunzi wote kusoma kwa bidii hususan wa kidato cha nne ambao wanatarajia kufanya mitihani yao mwezi Novemba.
Miradi mingine ambayo amekagua ni pamoja na kikundi cha vijana cha crossover kilichopatiwa mkopo wa shilingi milioni 50,ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ilemela, ujenzi wa ofisi ya kata ya nyasaka, zahanati ya Nyakato na mradi wa barabara ya Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongolo (Km 9) ambapo amehimiza ukamilishaji wa miradi hiyo ili ilete manufaa kwa wananchi.
#NTTupdates