×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI 500 WAJIANDIKISHA KUHAMA NGORONGORO.

Na Mwandishi wetu Dodoma.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi amesema wananchi 500 tayari wamejiandikisha na uthamini wa mali zao umefanyika kwaajili ya kuhama kwa hiari katika eneo la Ngorongoro kuelekea Msomera.

Matinyi ameyasema hayo leo Disemba 15 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Serikali imechukua hatua ya kuwapa elimu wananchi ili wahame kwa hiari bila kutumia nguvu yoyote huku akisema maendeleo waliyofikia mpaka sasa wanasubiri wakati wowote hasa mwishoni mwa mwaka huu 2023 nyumba nyingine zitakabidhiwa ili wananchi waweze kuhama.

#NttUpdates