×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI WATAKIWA KUKATAA RUSHWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA

Na Mwandishi wetu.

WANANCHI wa Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha wamehimizwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika nchini mwezi Novemba 2024 huku wakitakiwa kukemea na kukataa vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.

Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Eliakimu wakati akizindua klabu ya wapinga Rushwa shule ya msingi Monic kata ya Engariselo Wilaya ya Ngorongoro Julai 25, 2024.

Mnzava amewakumbusha wananchi kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa ni uchaguzi wa kisheria ambapo wananchi wanajukumu kubwa sana la kuchagua viongozi wenye sifa za kuwaongoza na wenye uzalendo wa nchi yake kwa kuwatumikia na siyo anayetoa rushwa.

Aidha amewapongeza wanafunzi wa klabu ya wapinga rushwa na kuwasisitiza walimu kuongeza nguvu ya kuwafundisha watoto hao masuala ya haki na rushwa.

NTTupdates