Na Mwandishi wetu.
Watu wanne, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Magufuli, Cathbert Julius (42).
Watuhumiwa wanaohusishwa kutenda tukio hilo ni Nyarukamo Mugasa (42) Mfanyabiashara, Aron Elias (35) Mkulima, Octavius Silvery (25) Dereva Bajaji na Bokeye Joseph (17) Utingo wa Bajaji wote Kwa pamoja ni wakazi wa Manispaa ya Geita mkoani Geita.
Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema kuwa watuhumiwa walitenda tukio hilo mnamo julai 5, mwaka huu majira ya saa mbili usiku ambapo walimvamia Mwalimu Cathebete Julius wakati alipokuwa akitengeneza bajaji yake aina ya Sinoray yenye namba za usajili MC 337DLG ambayo alikuwa akitumia kusafirishia Mifugo wanne aina ya Nguruwe kuelekea Geita Mjini.
Jeshi la Polisi limesema bajaji hiyo ilipata hitilafu eneo la Mkongolo wakati Mwalimu Cathbert akitengeneza ndipo ghafla akavamiwa na kikundi Cha wahalifu na kumjeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Jeshi la Polisi limeongeza kuwa ilipofika Julai 6, 2025 majira ya saa 5 asubuhi Mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa kandokando ya barabara ya lami eneo la kidongo chekundu huku bajaji pamoja na nguruwe vyote Kwa pamoja vimepata.
Jeshi la Polisi limesema kuwa linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo na watuhumiwa waliotenda tukio hilo watafikishwa mahakamani Kwa mujibu wa sheria.
Ametoa wito Kwa Wananchi wote kushirikiana bega kwa bega na Jeshi la Polisi katika kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu.
#NTTupdates