×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WASHIRIKI WAMWAGIKA RUANGWA MARATHON 2024

Na Mwandishi wetu.

Ikiwa msimu wa pili wa Ruangwa Marathon 2024, idadi ya washiriki imeendelea kuongezeka kwa kasi ambapo mpaka leo Septemba 12, 2024 washiriki zaidi ya 5000 wamejiandikisha kwenye mbio hizo.

Mgeni rasmi wa shughuli nzima ya Ruangwa Marathon, atakuwa Mh. Kassim Majaliwa ambae ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa.

Mbio hizo zitafanyika siku ya Jumamosi Septemba 14, 2024 na zitakuwa na umbali wa KM 5, KM 10 na KM 21 kwa washiriki na zitaanzia kwenye uwanja wa Madini na kuishia kwenye uwanja huo huo wa Madini.

#NTTupdates