×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI MWANZA 39 WAJERUHIWA

Na Mwandishi wetu.

Watu watano wamefariki dunia na wengine 39 kujeruhiwa, katika ajali iliyosababishwa na mabasi mawili kugongana eneo la Ukiriguru majira ya saa 12 asubuhi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ambayo imehusisha gari kampuni ya Nyehunge lilikua linatokea Mkoani Morogoro kuja Mkoani Mwanza lenye namba za usajili T281 EFG na basi kampuni ya Asante Rabi lenye namba ya usajili T458 DYD

Akizungumza eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa amesema pamoja na vifo hivyo majeruhi katika ajali hiyo ni 39 ambao wanapatiwa matibabu kwenye Hospitali iliyo karibu na eneo hilo.

#NTTupdates