
Jeshi la polisi kikosi cha Reli Nchini limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 77 wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya jinai ikiwemo kuhujumu miundombinu ya Reli na wizi wa mali za shirika.
Akitoa taarifa ya oparesheni iliyofanywa na jeshi hilo katika maeneo mbali mbali nchini Kamanda wa polisi kikosi cha Reli nchini Matride Kuyeto amesema wamewakama watu hao katika mkoa wa Dodoma wakituhumiwa kuiba nguzo 44 zinazoshikilia fensi ya SGR.

Matride pia amesema kuwa katika mkoa wa Mwanza vimekamatwa vifaa mbali mbali vya mradi kwenye ujenzi wa kipande cha Mwanza Isaka ikiwemo Madumu 105 yenye mafuta ya Diseli Pamoja na nondo 461.
Aidha Kamanda Matride ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo hivyo ikiwa ni Pamoja na wafanyabishara wanaonunua vyuma chakavu kuepuka na ununuzi wa vyuma vya mali ya shirika la Reli .




NTTUPDATES