×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

“WATUMISHI MADINI FANYENI KAZI KWA BIDII KUCHOCHEA AGENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA”-KIRUSWA

Na Mwandishi wetu.

Wafanyakazi wa Wizara ya Madini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kuharakisha agenda ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia madini mkakati yanayopatikana nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 28,2024 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, wakati akifungua mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.

“Sekta ya madini ni Jicho la Serikali na Madini mkakati tuliyonayo yanapaswa kuchochea maendeleo ya nchi hasa katika eneo la Nishati safi ya kupikia kwani Dunia kwa sasa inaitazama Tanzania kama mfano wa kuigwa katika eneo hilo,

“Dkt. Kiruswa amewataka pia watumishi hao kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kuachana na vitendo vinavyoweza kudhoofisha maendeleo ya Sekta ya madini ikiwemo kujiepusha na vitendo vya Rushwa.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa Serikali imewapa wajibu wa kufanya tafiti kwa kutumia taasisi ya GST ambapo mpaka sasa wameshafanya kwa asilimia 16 lengo likiwa ni kufikia asilimia 50 ifikapo 2030.

#NTTupdates