×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WINGA WA SAUDI ARABIA ADONDOKA GHOROFANI

Na Mwandishi wetu.

Nyota wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia Fahad Mosa’ed Al Muwallad (30) anayekipiga kunako klabu ya Al- Shabab inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Pro League amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kudondoka kutoka ghorofa ya pili akiwa nyumbani kwake na kupelekea madhara hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi, kuwa Al-Muwallad alidondoka kutoka ghorofani na hali yake siyo nzuri huku wakiweka wazi uchunguzi kuwa bado unaendelea wakishirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi ili kufahamu chanzo cha tukio hilo.

#NTTupdates