×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

YANGA SC YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

Na Mwandishi wetu.

Kikosi cha klabu ya Young Africans SC, kimewasili nchini Ethiopia kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ambapo watacheza dhidi ya CBE ya Ethiopia.

Mchezo huo utapigwa Septemba 14, 2024 siku ya jumamosi ambapo Young Africans SC, wameweka wazi kuwa watafanya vizuri kwenye mchezo huo kama kawaida yao na kufuzu hatua ya makundi.

Young Africans SC, ndiye muwakilisha pekee wa Tanzania kwenye ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya Azam FC kuondolewa kwenye michuano hiyo.

#NTTupdates