×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ZAIDI YA VIKUNDI 110 VYANUFAIKA NA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI

Na Mwandishi wetu.

Jumla ya Vikundi 111, vikijumuisha makundi maalumu ya Wanawake, Vijana pamoja na Watu wenye Ulemavu vimeweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 1,156,750,000 Wilayani Geita, ikiwa ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi.

Hayo yamebainishwa wakati wa hafla ya ugawaji wa mikopo hiyo makao makuu ya Halmashauri ambapo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amesema kuwa bado uhitaji wa mikopo hiyo inayotolewa na serikali pasi na kuwa na riba ni mkubwa kwa kuwa bado wananchi wana dhamira ya kujikwamua kiuchumi huku akiiagiza Halmashauri kuendelea na utaratibu wa kutenga fedha, kwajili ya kuinua maisha ya wananchi.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wanufaika kuibua miradi yenye tija hili fedha walizozipata ziweze kuwasaidia kwenye malengo yaliyokusudiwa na mikopo hiyo iweze kurudi kwa wakati hili kusudi na wengine waweze kukopa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Magaro amesema kuwa suala la utoaji wa mikopo hiyo ni kubwa hususani kwenye nyanja ya kuiingizia kodi serikali kwa kuwa inachangiia mzunguko wa fedha kuongezeka ndani ya Halmashauri huku akiwataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vizuri.

#NTTupdates