×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ZAIDI YA WAGONJWA 450 WAPATIWA HUDUMA YA UPASUAJI WA MACHO BURE ARUSHA

Na Mwandishi wetu.

Zaidi ya wananchi 450 kutoka maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Arusha wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mtoto jicho iliyotolewa bure kupitia kampeni ya afya iliyoendeshwa na madaktari bingwa kutoka nchini Hispania.

Huduma hiyo iliyolenga kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini inafanyika katika hospitali ya Wilaya ya Meru na kushuhudia idadi kubwa ya wananchi wakijitokeza kwa wingi kwaajili ya kupatiwa huduma hiyo kitu ambacho kimeleta furaha kwa wananchi wengi waliokuwa wakikumbwa na changamoto ya macho.

Mnamo leo Aprili 18. 2025, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ametembelea hospitali hiyo na kujionea jinsi wagonjwa mbalimbali wanavyoendelea kupatiwa huduma hiyo lakini pia kuwajulia hali ya afya zao.

Aidha, Makonda amewapongenza watoaji wa huduma hiyo akiwashukuru kwa namna ya upekee kwani wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii ya watu wa chini wasiokuwa na uwezo wa kulipia huduma hiyo hospitalini lakini kupitia uwezeshaji wao wa utoaji huduma ya mtoto wa jicho imeweza kurejesha furaha kwa wananchi hao waliokuwa wakihitaji hudama hiyo.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi waliokwisha patiwa huduma hiyo wameelezea jinsi waliyonufaika na ubora wa huduma hiyo na kwasasa wamepata matumaini mapya ya kuona vizuri tena kama mwanzo na kutoa shukrani zao kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwezesha hilo kutokea bila ya malipo yoyote.

#NTTupdates.