×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ZUNGU AIPONGEZA NMB KWA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO

Na Mwandishi wetu.

NAIBU Spika, na Mbunge wa jimbo la Ilala jijini Dar es salaam, Mussa Azzan Zungu ametembelea maonyesho ya wafanyabiashara wa kariakoo yajulikanayo kwa jina la (Kariakoo Festival) yanayoendelea kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, na kuipongeza benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo nchini wanainuliwa kwa kuwezeshwa kimitaji.

Naibu Spika Zungu akiongea mara baada ya kutembelea maonyesho hayo ya (Kariakoo Festival) ambayo mdhamini mkuu wake ni Benki ya NMB, amewataka wafanyabiashara hao kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB kwao na kuhakikisha wakati wote wanakwenda na mahitaji ya wateja wao huku wakizingatia kuwa biashara ni ushindani inayohitaji ubora wa bidhaa, uaminifu pamoja na uharaka wa kumfikia mteja.

Kwa upande wao Benki ya NMB wakiwakilishwa na meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani Seka Urio, wamesema moja ya jukumu la benki ya NMB ni kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa na kila mtanzania anapata fursa ya kuchangia ukuwaji wa uchumi huo, ikiwamo wafanyabiashara wadogo na wakati, ndio maana benki ya NMB imeingiza sokoni bidhaa kama teleza kidigitali, QR CODE, pamoja na elimu ya Bima ili kumwezesha kila mjasiriamali na mfanyabiashara nchini kunufaika na bidhaa za benki hiyo.

Kariakoo Festival ambayo imekutanisha wafanyabiashara wa aina zote kutoka eneo la kariakoo, maonyesho yanayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam, yatadumu kwa wiki moja huku mdhamini mkuu wake akiwa benki ya NMB.

#NTTupdates