Na Mwandishi wetu.
Abiria wote nchini wametakiwa kupaza sauti zao pale waonapo madereva wakiendesha mwendo Kasi, ili kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari yoyote ya kuepusha ajali.
Kauli hiyo imetolewa Mkoani Kagera na Kamanda wa Kikosi Cha usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) William Mkonda, wakati wa Oparesheni maalumu ya kuwabaini madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
Oparesheni hiyo , inalenga kudhibiti matukio ya ajali za barabarani ambapo madereva wamepimwa ulevi kabla ya kuanza Safari, ukaguzi wa mifumo ya usukani, tairi, bodi pamoja na taa hili kujihakikishia usalama wa chombo Cha usafirishaji abiria.
#NTTupdates