×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

ACT KUENDELEA NA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR

Na Mwandishi wetu.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, OTHMAN MASOUD, ameeleza kuwa ACT-Wazalendo imekubali kuendelea kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa ajili ya maridhiano.

Amesema wanaendelea na hilo ingawa baadhi ya makubaliano muhimu, ikiwemo Tume Huru ya Uchunguzi, mauaji ya 2020 na vitambulisho vya Uzanzibari, hayajatekelezwa.

Na kisha akaeleza kuwa Viongozi wa Dini nchini wanayonafasi kubwa ya kusikika zaidi hata kwa baadhi ya Watawala ambao hawawasikilizi Wananchi.

Amesema Viongozi wa dini wananafasi ya kutumia sauti zao kupigania haki na amani ya kweli, alizozitaja kuwa ndizo nguzo za maendeleo ya taifa.

Amesema haijalishi nani atashinda, kilicho muhimu ni haki kutendeka na maamuzi ya wananchi yaheshimiwe,” amesema.

Ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Mhashamu Augustine Shao.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amesisitiza kuwa amani hupatikana endapo haki itasimamiwa mapema.

Kwa upande wake Askofu Shao amesema amani ya kweli hutokana na kila mtu kupata haki yake, akibainisha kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekuwa nguzo ya utulivu na kichocheo cha uchumi kupitia utalii.

#NTTUpdates