×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

AHMED ALLY AWATOA HOFU WANASIMBA INSHU YA TSHABALALA

Na Mwandishi wetu.

Afisa Habari wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amewatoa shaka mashabiki na wadau wa klabu ya Simba SC juu ya kuondokewa na Nahodha wao Mohamed Hussein Tshabalala.

“Kwanza ifahamike kuwa tunampenda, tunamheshimu Mohamed Hussein na hiyo itabaki milele. Ulikuwa ni muda sahihi kwa Tshabalala kuondoka Simba, na muda sahihi kwa Simba kuachana na Tshabalala.

Katika hili agano, hakuna hasara kwa Simba wala kwa Tshabalala. Kila mmoja amenufaika na maamuzi haya”.

Ahmed Ally amewaeleza mashabiki wa klabu hiyo akiwataka watulie na kutokuwa na hofu kwa kuondokewa na Nahodha wao.

Baadhi ya mashabiki wamehuzunishwa na Nahodha huyo kuondoka wakiamini Bado alikuwa na mchango ndani ya klabu lakini ujumbe wa semaji Ahmed Ally kwa mashabiki ni wazi kuwa klabu hiyo imejipanga kuziba pengo la nyota huyo na kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.

Nahodha Mohamed Hussein aliwaaga mashabiki wa Simba SC siku jana akiwashukuru kwa kuwa pamoja kwenye nyakati zote kwa miaka 11.

#NTTupdates