×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

AL AHLY YAMPIGA FAINI NA KUMUONDOA KIKOSINI EMAN ASHOUR

Na Mwandishi wetu.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Al Ahly SC ya nchini Misri imempiga faini na kumuondoa kikosini kiungo mshambuliaji Eman Ashour Metwally Abdelghany (26) baada ya utovu wa nidhamu kwenye klabu hiyo.

Kiungo huyo alikasirishwa na kitendo cha kuachwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya Mabingwa (CAFCL) dhidi ya Stade d’Abidjan na Al Ahly SC ilishinda magoli 4-2.

Pia Kiungo huyo alibishana na kukataa maamuzi ya nahodha wa kikosi hicho goli kipa Mohamed Elshanawy na kupelekea kupigwa faini ya Paundi Milioni moja za Misri (Milioni 52 za Tanzania) na kuondolewa kwenye mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzie kwa muda wa wiki moja hivyo kulazimika kufanya mazoezi peke yake.

Al Ahly SC imekuwa na muendelezo wa kutoa adhabu na faini kwa wachezaji wanaofanya vitendo ambavyo vinaashiria utovu wa nidhamu kwenye klabu hiyo.

#NTTupdates