Na Mwandishi wetu.
Mlinzi wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Tunisia Ali Maaloul (35) ambaye aliwahi kutamba na Mabingwa wa kihistoria wa ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Al Ahly ya Misri ametambulishwa rasmi na klabu yake ya utotoni ya CS Sfaxien inayoshiriki ligi kuu nchini Tunisia.
CS Sfaxien ndiyo timu iliyomlea mlinzi huyo wa kushoto toka akiwa kijana mdogo, ambapo aliondoka klabuni hapo mwaka 2016 akiwa na umri miaka 26 baada ya Al Ahly kuvutia na uwezo wake wa kuzuia, kutengeneza nafasi za kufunga kwa wachezaji wenzake na umahiri wa kuweka mpira golini.
Al Maaloul ameichezea Al Ahly kwa miaka tisa (9) kwenye Michezo 292 akifunga magoli 51 na kutoa assist 85 katika mashindano yote ambayo klabu hiyo ilishiriki wakati akiwatumikia huku akitajwa, kuwa miongoni mwa walinzi wenye uwezo mkubwa dimbani.
#NTTupdates