Na Mwandishi wetu.
Mahakama ya Wilaya ya Sengerema imemuhukumu kifungo Cha miaka 30 jela Lindwa Clement Balthazari(30) kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 kutoka Shule msingi mwakilima ambaye jina lake limehifadhiwa.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi ndeko Dastan Ndeko katika kesi ya namba 31961/2024 Baada ya ushahidi wa pande zote mbili kuthibishwa basi na shaka mbele ya mahakama hiyo.
Mahakama ilithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa Hilo nyumbani kwake kwa kumrubuni mtoto huyo salon kwake na kumbaka kinyume Cha Sheria vifungu namba 130(1), 130(2)(a) na 131(1).
Ya kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo ya 2022.Mashahidi wanne waliwasilishwa upande wa mashtaka wakiwemo mhanga na Daktari aliyethibitisha pasi na shaka kuwa mtoto huyo alibakwa na mahakama kutoa hiyo ili hiwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo kuacha Mara moja.
#NTTupdates