
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kuwakamata Askari mgambo watatu wanaodaiwa kumpiga hadi kumuuwa mtu mmoja aitwaye Rashidy Masunga aliyekuwa fundi simu
Akizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu kamishna Wilbrod Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Machi 20 mwaka huu ambapo inadaiwa siku hiyo ya tukio majira ya jioni katika mtaa wa Misheni kata ya Pamba wilaya ya Nyamagana, mgambo hao walimtilia shaka marehemu kuwa anauza dawa za kulevya aina ya mirungi
Kamanda Mutafungwa ameongeza kuwa baada ya Mgambo hao kumtilia shaka Rashidy na kisha Rashidy kushtuka kama anafatiliwa ndipo wakaanza kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata
