Na Mwandishi wetu.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Balozi Andrew Lentz amefika Jijini Arusha na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla leo Alhamisi Septemba 11, 2025 wa lengo la kuendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya Jiji la Arusha na pamoja na Tanzania kwa ujumla wake.
Katika mazungumzo hayo, CPA Makalla amemshukuru Balozi Lentz kwa ushirikiano na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Tanzania hususani katika sekta ya utalii, akieleza kuwa Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla ni wanufaika wa idadi kubwa ya watalii kutoka nchini Marekani, huku akimsisitiza kuendelea kuwashawishi raia wengine wa Marekani kuja kufanya utalii na kuwekeza nchini kutokana na uwepo wa hali shwari ya usalama na amani.”
Mkoa wa Arusha una utulivu mkubwa wa kisiasa, amani, usalama unaosababisha wananchi wetu kuendelea kujikita kwenye shughuli zao za maendeleo hivyo niwahakikishie raia yeyote wa Marekani na Mataifa mengine hawana sababu ya kuwa na wasiwasi wa kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana Arusha ama kuja kuwekeza na kufanya biashara. Amesema Makalla.
#NTTupdates.