×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BARCELONA YAMUONGEZEA MKATABA HANSI FLICK

Na Mwandishi wetu.

Mabingwa wa ligi kuu ya Hispania (La Liga) FC Barcelona imemuongezea mkataba Kocha mkuu wa kikosi hicho Hansi Dieter Flicks (60), raia wa Ujerumani ambao utamalizika mwaka 2027.

Mjerumani huyo ambaye ameweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye klabu hiyo baada ya kuiwezesha FC Barcelona kutwaa mataji matatu ambayo taji la ligi kuu (La Liga), Copa del Rey na Supercup ya Hispania mbele ya mahasimu wao Real Madrid.

Rais wa klabu hiyo Joan Laporta na Mkurugenzi wa ufundi, Anderson Deco wameamua kumuongezea mkataba Kocha huyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho na namna alivyoweza kuwatumia wachezaji wachanga kama Pau Curbasi, Fermin Lopez, Gerard Martin, Lamine Yamal, Ferran Torres Alejandro Balde na wengineo kuwa na kiwango cha kuridhisha na kusaidia timu hiyo kubeba taji la 28 la ligi hiyo.

Hansi Flick alijiunga na FC Barcelona mwanzoni mwa msimu ambapo ameiongoza klabu hiyo kwenye michezo 59, akishinda michezo 43 Suluhu michezo 7 na kupoteza michezo 9, huku alifanikiwa kuipeleka klabu hiyo nusu fainali ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) ambapo walitolewa na Inter Milan kwa jumla ya magoli 7-6.

#NTTupdates