×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BENJAMIN MKAPA YAFUNGIWA KWA MUDA NA CAF

Na Mwandishi wetu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefungia kwa muda dimba la Benjamin Mkapa lililopo Dar es Salaam kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake.

CAF imeelekeza maboresho ya uwanja huo yafayike haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepuka Uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry ya Misri iliyopangwa kuchezwa kwenye uwanja huo Aprili 9, 2024 uhamishiwe uwanja mwingine hivyo TFF kuwasilisha jina la uwanja mbadala ifikapo Machi 14, 2025.

CAF imepanga kufanya ukaguzi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 20, 2025 ili kuona maboresho yaliyofanyika kabla ya kufanya maamuzi ya matumizi yake.

#NTTupdates