Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Tottenham Hotspur imempiga marufuku kiungo wao Rodrigo Bentancur Colman (27) raia wa Uruguay baada ya kumtusi nahodha wa kikosi hicho Son Heung-min (32) raia wa Korea Kusini kupitia matamshi yake ya kibaguzi wakati akifanya mahojiano
.” Mchezaji gani? Son au binamu zake Son maana wote wanaonekana sawa kama kwenye kipindi cha televisheni Cha Por la Camiseta”.
Alisema Bentancur wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja nyumbani kwao Uruguay.
Nyota huyo, pia alishtakiwa kwa madai ya kukiuka sheria za FA mwezi Septemba kutokana na mahojiano yake aliyoyafanya na kituo cha TV nyumbani kwao Uruguay na kufungiwa mechi 7 na faini ya Paundi 100,000 (Milioni 335) baada ya kukutwa na hatia ingawa anaruhusiwa kucheza michezo ya mashindano ya kimataifa ya UEFA EUROPE League.
Licha ya Bentacur kuomba msamaha kwa kitendo hicho kupitia mtandao wa kijamii lakini ataendelea kutumika adhabu hiyo.
#NTTupdates