×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BILLION 59 KUJENGA BARABARA SAME – MKOMAZI

Na Mwandishi wetu.

Katibu wa Halmashauri Kuu ( NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema kuwa Serikali imetoa jumla ya kiasi cha fedha shillingi billion 59 kwaajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 35 kutoka Same – Kisiwani – Mkomazi kwa kiwango cha lami.

Makalla amesema hayo leo Juni 11, 2025 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano uliofanyika katika Kata ya Ndugu Jimbo la Same Mashariki Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.

Ameeleza hayo wakati akigusia taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecela iliyoainisha miradi ya mendeleo iliyotekelezwa katika jimbo hilo katika maeneo mbalimbali na ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya miradi iliyopo katika utekelezaji.

Aidha, ameongeza kwa kusema takribani kilometa 100 zinazohitajika kujengwa hadi ujenzi wa mradi huo utimie lakini hajitajengwa kwa wakati mmoja bali zitakuwa zikijengwa kwa awamu kwani barabara hiyo ni miongoni mwa barabara zilizopigiwa kelele sana na viongozi pamoja na wananchi.

#NTTupdates.