×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BINGWA WA LIGI KUJULIKANA JUNI 25.

Na Mwandishi wetu.

Baada ya Mnyama Simba SC pamoja na Wananchi Young Africans SC,kupata ushindi kwenye michezo yao ya mzunguko wa 30 wa ligi kuu ya NBC, bingwa rasmi wa ligi kuu msimu huu atajulikana siku ya Jumatano Juni 25, 2025 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ushindi wa leo umewafanya Young Africans SC kufikisha alama 79, wakisalia nafasi ya kwanza huku watani wao Simba SC wakifikisha alama 78 wakiwa nafasi ya pili, hivyo mchezo wa mwisho kati yao ndio utaamua nani awe bingwa wa msimu huu huku Mnyama Simba SC atalazimika kushinda Mchezo huo.

#NTTupdates