×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BRAZIL YAMFUTA KAZI DORIVAL KISA ARGENTINA

Na Mwandishi wetu.

Shirikisho la soka nchini Brazil (CBF), limemfuta kazi Kocha wa Timu ya Taifa ya Brazil, Dorival Silvestre Junior (62), baada ya Taifa hilo kupokea kichapo kizito cha magoli 4-1 kutoka kwa Argentina kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia mwaka 2026.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mabingwa mara tano wa kombe hilo Brazil, kutamba kuwa watapata ushindi kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Argentina lakini mambo yalibadilika na kushuhudia wakipokea kichapo kizito huku lawama zikienda kwa Kocha wa kikosi hicho Dorival Junior.

Dorival Junior alianza kukinoa kikosi Cha Brazil, Januari 2024 akitokea klabu ya Sau Paulo ambapo ameiongoza Brazil kwenye michezo 16 akishinda michezo 7, sare michezo 7 na kupoteza michezo 2.

Brazil ipo sokoni kusaka Kocha mpya ambae atakuja kukinoa kikosi hicho huku majina yanayotajwa zaidi ikiwa ni pamoja na Carlo Ancelott wa Real Madrid na Jorge Jesus wa Al Hilal ya Saudi Arabia.

#NTTupdates