Na Mwandishi wetu.
Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Miguel Borges Fernandes (30) na mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo (39) wameweka rekodi ya kuwa wachezaji pekee kutoka Taifa la Ureno kuchangia magoli zaidi ya 100 kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL)Bruno Fernandes amechangia magoli 155 akifunga magoli 83 na assist 72 kwenye klabu yake ya Manchester United toka ajiunge nayo 2020.
Cristiano Ronaldo pia amechangia magoli 103 na assist 39 kwenye vipindi tofauti ambavyo ameitumikia Manchester United kwenye ligi kuu ya Uingereza huku akifunga magoli 145 kwenye mashindano yote ambayo akiitumikia klabu hiyo.
Wachezaji wengine kutoka Ureno waliochangia magoli kwenye vilabuni vyao EPL niLuis Carlos Almeida da Cunha akijulikana kama NANI akiwa Manchester United alichangia magoli 86 (Assist 60 na magoli 26)Bernardo Silva kiungo mshambuliaji wa Manchester City mpaka sasa amechangia magoli 64 (assist 30 na magoli 34) na wa Tano ni ni Diogo Jota kutokea Liverpool akichangia magoli 62 (assist 42 na magoli 20).
#NTTupdates