×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

CHANGAMKIENI FURSA HII YA MSAADA WA KISHERIA – THADAYO

Na Mwandishi wetu.

Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Thadayo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo ya msaada wa kisheria iliyoletwa kwao na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili ili waweze kusikilizwa na kutatuliwa kero pamoja na changamoto mbalimbali za Kisheria bila ya malipo.

Thadayo amesema hayo leo Machi 28, 2025 kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Kizito Mhagama wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia uwanja wa Ngarenaro Jijini Arusha.

Sambamba na hilo, Thadayo amewataka Mawakili, Wanasheria kutoka Serikalini na Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) watakao hudumia wananchi hao kuhakikisha wanazingatia maadili ya taaluma zao ili kutenda haki kwa kila mtu.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo inatarajiwa kudumu kwa muda wa siku kumi (10) ndani ya mkoa wa Arusha.

#NTTupdates.