×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

CUNHA ANAITAKA MANCHESTER UNITED

Na Mwandishi wetu.

Mshambuliaji wa klabu ya Wolverhampton Wanderers, Matheus Santos Carneiro da Cunha (25), raia wa Brazil ameweka wazi kuwa mpango wake ni kujiunga na mashetani Wekundu, Manchester United msimu ujao kwa dau la Paundi Milioni 62.5.

Nyota huyo ambaye vilabu kadhaa barani Ulaya vimekuwa vikihitaji huduma yake kama Arsenal kutokana na kiwango Bora lakini nyota huyo amezipiga chini ofa hizo.

Cunha amekuwa na msimu mzuri ndani ya Wolves ambapo amecheza michezo 31 akifunga magoli 16 na kutoa assist 4 kwenye mashindano yote ambayo klabu hiyo imeshiriki msimu huu.

#NTTupdates