×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DABO NDANI YA AS VITA DR CONGO

Na Mwandishi wetu.

Pomboo Weusi wa jiji la Kinshasa nchini DR Congo, AS Vita klabu imemtambulisha Kocha wao mpya Youssoupha Dabo (44) raia wa Senegali kuwa Kocha mkuu wa kikosi hicho msimu huu.

Dabo ambaye aliinoa Azam FC msimu uliopita na kuiongoza klabu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu NBC 2023/2024 na baadae kutimuliwa na matajiri hao wa Chamazi, baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Dabo amechukua nafasi ya Kocha Mkongomani Raoul Shungu ambaye alikuwa Kocha wa muda wa kikosi hicho.

#NTTupdates